Tembelea Israel kupitia Egypt.

Ratiba ya kutembelea Israel kupitia Egypt!

  • Siku ya kwanza

Kuwasili na kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Cairo kutokea Dar es salaam ambapo tutakamilisha taratibu za uhamiaji na hatimaye kuelekea katika Hoteli mjini Cairo tayari kwa kupatiwa vyumba vya kupumzika na kupata kifungua kinywa kwenye muda wa saa 5:00 asubuhi. Baada ya hapo ni kutembelea GIZA PYRAMIDS MEMPHIS, SAQQARA EGYPT MUSEUM na OLD COPTIC CAIRO. Siku nzima itakuwa ni kutembelea jiji la Cairo ambapo tutafika katika Pyramids na Sphinx, kutembelea Makumbusho na Makanisa ya zamani ya Cairo. Baada ya hapo ni kurudi Hotelini kwa ajili ya chakula cha usiku na kulala.

  • Siku ya pili

KUONDOKA CAIRO KUELEKEA TABA – EILAT

Baada ya kifungua kinywa jijini Cairo, itakuwa ni safari ya kuelekea Taba-Eilat mpaka muda wa jioni tutawasili moja kwa moja katika katika Hoteli ambapo tutapata chakula cha jioni na baadaye kulala.

  • Siku ya tatu

MASADA – DEAD SEA – JERUSALEM

Mapema asubuhi itakuwa ni kutembelea msitu unaongua na mahali ambapo Moses alipokea amri 10 (Kupanda mlima sinai). Baadae kurudi katika hoteli kwa ajiri ya mapumziko na kifungua kinywa na baadae kuelekea TABA kwa chakula cha jioni na kulala.

  • Siku ya nne

YERUSALEM YA KALE

Siku hii ni kutalii Eliat, kutembelea kando kando za bahari ya Chumvi (Dead Sea) hadi msingi wa Masada, Ngome ya mwisho ya Jewish Zealots dhidi ya Warumi. Kutakuwa na kutumia usafiri wa Cable kutembelea eneo maarufu la Archaeology (Famed Archaeological site), kuona Hekalu la Herode, sinagogi la kale pamoja na Bathhouse. Tutatumia tena usafiri wa gari hadi Bahari mfu (Dead Sea) baada ya kushuka katika cable. Hapo tutapata nafasi ya kuogelea na kufurahi katika maji ya kipekee ya Bahari mfu. Kabla ya kuanza safari ya kuelekea Yerusalemu kutakuwa na kutalii Qumran, sehemu ambayo jamii ua Ki-Essene iliandika juu ya bahari mfu. Baadae kuelekea Jericho kupanda mlima wa majaribu kwa kutumia usafiri wa cable. Tutapitia pia maeneo ya Zakaria ambapo tutaona vilima vya Yudea ili kufika mji wa amani wa Yerusalem na nyumba ya dini tatu. Hapo tutapata chakula cha jioni na kulala katika hoteli ya Prima Park.

Asubuhi yake baada ya kifungua kinywa tutapanda mlima kwa ajili ya mtazamo wa kimaajabu na kuweza kuona mji mzima wa Yerusalem. Tutaweza pia kuona eneo la kiasili la jumapili ya Matawi kuelekea Kanisa la mataifa yotena kufika katika bustani ya Gethsemane. Hapo tutaelekea pia mlima Zion kupitia Bonde la Kidron na kutembelea chumba cha karamu ya mwisho na kaburi la Daudi. Tutaendelea kutembea na kuona mji wenye kuta na kuangalia kuta za magharibi na Cardo. Tutafurahia mtazamo wa kipanorama wa mwamba katika mlima wa Temple ndani ya kasri la Kikristo la kanisa la Mtakatifu Anne, Ecce Homo, Hekalu la Antonia na kanisa la kaburi takatifu la Sepulcher na mwisho wa siku kupata huduma ya komunio kwenye bustani ya kaburi (Gordon’s Calvary). Baadae ni kupata chakula cha jioni na kulala katika hoteli ya Prima Park.

  • Siku ya Tano & Sita

KUTALII MAENEO YA TIBERIA, KAISARIA, CARMEL MEGGIDO, CAPERNAUM

Mapema asubuhi baada ya kifungua kinywa, tutasafiri kwa gari kupitia bonde la mto Jordan na kuanza siku kwa kutembea kwa mashua katika bahari ya Galilaya, Hapo tutaeleka hadi Kaperanum ili kuona mlima wa kugeuzwa wa Tabori, eneo la kubatizia na kuendelea hadi Tabgha, eneo la miujiza ya mikate na samaki na masalia yake kutoka karne ya 5, Byzantine basilica ikifuatiwa na kutembelea Nazaret Viakana ya Galilaya, mahali ambapo miujiza ya kwanza ya Yesu Kristo alipoweza kubadilisha maji kuwa mvinyo.

Tutafika kwa gari katika mlima Beatitudes, sehemu ya mahubiri juu ya mlima. Hapa kutakuwa na muda wa tafakari binafsi (meditation). Safari itaendelea hadi Bainas kupitia Galilaya ya juu, milima ya Golan na kurudi Yerusalem. Tutapata chakula cha jioni na kulala katika hoteli ya Prima Galil.

  • Siku ya Saba

JERUSALEM MPYA NA BETHLEHEM

Baada ya kifungua kinywa, kutakuwa na utalii wa mji mpya wa Yerusalem kuanzia kaburi la kitabu katika makumbusho ya Israel ambapo michoro ya bahari mfu huonyeshwa. Pia tutaona mfano mdogo wa Yerusalem ya kale. Mchana kutakuwa na ziara katika hekalu la Manger kule Bethlehem na kutembelea kanisa la kuzaliwa Yesu, Shepherd Field na Milk Grotto. Baadaye jioni ni chakula na kulala katika Hoteli Prima Park, Yerusalem.

  • Siku ya nane

EIN KAREEM – YAD VASHEM

Safari ya kuelekea Ein Kareem itaanza baada ya kifungua kinywa. Hii itakuwa ni kutembelea Kanisa la Visitation, Mtakatifu Petro Grotto na kuendelea na safari ya Yad Vashem hadi Holocaust. Baada ya hapo ni kurudi hoteli ya Prima Park, Yerusalem kwa ajiri ya chakula cha jioni na kulala.

  • Siku ya Tisa

JERUSALEM – TABA

Safari ya kuelekea Taba kutokea Yerusalem ittanza baada ya kifungua kinywa. Baada ya kufika Taba mpakani ambapo tutakamilisha taratibu za uhamiaji na hatimaye kuelekea katika Hoteli kwa ajili ya kula na kulala.

  • Siku ya Kumi

KUONDOKA CAIRO

Baada ya kifungua kinywa tutaelekea uwanja wa ndege wa Cairo tayari kwa safari ya kuondoka.

About the Author

By allydege / Administrator, bbp_keymaster

Follow allydege
on Dec 10, 2016

Categories

December 2017
M T W T F S S
« Dec    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031

Cordial Socials